Update:

01 August 2016

Papa Francis: Messi Ni Bora Kuliko Pele Na Maradona


 Lionel Messi-Pele-Diego Maradona-Christiano Ronaldo
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis hajulikani kama mshabiki wa soka. Hata hivyo ana sifa ya kuusemea moyo. Amekuwa hasiti kutoa maoni yake kuhusiana na masuala mbalimbali duniani. Na kwa sababu Papa ni raia wa Argentina taifa ambalo huthamini soka karibu na wanavyothamini dini, bila shaka alikulia akiona au hata kucheza soka kidogo.
Haishangazi kwamba alipoombwa maoni yake kuhusu mchezaji anayemuona kuwa bora zaidi ulimwenguni, alikuwa na la kusema. Jibu lake ni Lionel Messi raia wa Argentina anayechezea Barcelona.
Papa Francis ameulizwa swali hilo huko nchini Poland unapofanyikia Mkutano wa Vijana wa Kanisa Katoliki kuhusu nani ni bora kati ya Lionel Messi, Pele na Diego Maradona.Papa anasema mshindi wa tuzo 5 za Mchezaji Bora wa FIFA.
Mbali ya magwiji kama mfalme wa soka Pele na Maradona, Messi hupambanishwa na Christiano Ronaldo ambaye hivi karibuni ameshinda Kombe La Mataifa Ya Ulaya na Portugal huku Messi akishindwa kuiongoza Argentina katika michuano ya Copa America na kukubali kipigo mbele ya Chile. Messi alitangaza kustaafu kuchezea timu ya Taifa ya Argentina baada ya fainali za Copa America 2016 zilizofanyikia nchini Marekani.