Update:

17 August 2016

Mradi wa kuwaandikia watu nyimbo unanifanya niishi bila stress – Linex

Msanii wa muziki, Linex Sunday Mteja amesema mradi wake wa kuwaandikia watu nyimbo ndiyo mradi pekee kwenye muziki wake ambao unampatia pesa za uhakika.
Linex
 Linex amesema anaweza kujipa mapumziko kwenye muziki na kuishi maisha mazuri kwa kutegemea pesa za kuwaandikia watu nyimbo.
“Bado nawaandikia watu nyimbo, tena ni mchongo ambao unanipatia pesa nyingi sana,” alisema Linex. “Yaani naweza hata nikapumzika kufanya show nikawa nategemea pesa za kuwaandikia watu nyimbo, kwa hiyo ni kitu ambacho kinanipiga tafu sana, naishi bila hata stress,”
Muimbaji huyo anayefanya vizuri na wimbo ‘Hewala’, amesema wanandoa ni moja kati ya wateja wake wakubwa katika mradi huyo.
Pia muimbaji huyo amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio wa video yake mpya ya wimbo ‘Hewala’.
source:bongo5