Update:

17 August 2016

Malalamiko ya wanachama wa Yanga Africans yafika TFFShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea malalamiko mbalimbali ya wanachama wake, yakiwamo ya wanachama watatu wa Young Africans waliofukuzwa kwenye Mkutano wa Dharura wa wanachama uliofanyika jijini Dar es Salaam Agosti 26, 2016.
tff
Wanachama hao Ayoub Nyenzi, Hashim Abdallah na Salum Mkemi wanapinga uamuzi wa kufukuzwa na wanaomba chombo cha sheria cha hadhi ya wanachama na katiba kupitia kamati ya maadili kuangalia suala hilo kwa kuwa limekiuka sheria katika uamuzi uliochukuliwa dhidi yao.
Wanadai kuwa Katiba Young Africans ya mwaka 2010, Ibara ya 22 inainisha taratibu za kuitisha mkutano wa dharura kipenglee namba 1-6, ibara ya 23 (1), (2) inaeleza akidi ya kutoa maamuzi ya mkutano mkuu.
Kadhalika wanadai Ibara ya 12 ya kusimamishwa uwanachama kipengele cha 1, 2, vinaeleza uvunjani mkubwa wa katiba ya wanachama, na wajibu wa kamati ya utendaji wa kutoa adhabu kwa mwanachama mkosaji, TFF imepokea malalamiko yao na itapeleka kwenye kamati husika.
Source: tff.or.tz