Update:

16 August 2016

Juuko kuuzwa Afrika Kusini

Klub ya Simba inatarajia kupata dola za marekani 100,000(zaidi ya Tsh. milioni 200)kwaajili ya kumuuza beki wake wa kati Mganda.

 Rais wa Simba Evans Aveva alisema kuwa tayari wameshafanya mazungumzo na wakala (jina linahifadhiwa) ambaye ameridhishwa na kiwango cha beki huyo anayeichezea pia Timu ya Taifa ya Uganda (Cranes).
Aveva alisema kuwa endapo beki huyo atafanikiwa kuondoka, nafasi ya ulinzi ya timu hiyo itapata pigo na tayari wameshamueleza kocha Joseph Omog kuanza kujipanga.
"Mazungumzo ya awali yameshafanyika na sasa kinachosubiriwa na barua ramsi, wakala wake anafanya kazi karibu na Micho (Milutin Sredojevic- Kocha Mkuu wa Cranes), hivyo haendi kufanya majaribio, ni kuanza kucheza moja kwa moja," alisema Aveva.
Aliongeza kuwa nafasi ya Juuko huenda ikazibwa na Novat Lufungo ambaye ameonekana kuiva zaidi tofauti na alivyokuwa msimu uliomalizika.