Update:

31 August 2016

DC ARUMERU: POSHO ZA MADIWANI ZIPUNGUZWE
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru  Alexander Pastory Mnyeti  amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kupunguza posho za Madiwani kutoka laki moja na ishirini (220,000) mpaka shilingi elfu themanini (80,000)za kitanzania na kutoa onyo kwa  Mkurugenzi atakye kiuka agizo hilo.

Akizungumza katika kikao kilicho wakutanisha wakuu wa idara mbalimbali kutoka Halmashauri ya Meru  pamoja na Halmashauri ya Arusha  amesema kuwa Madiwani hao wamekuwa wakipokea kiwango kikubwa cha posho na kuwaagiza  Wakurugenzi kupunguza kiasi cha posho hizo pamoja na fedha walizo kuwa wakipewa kama nauli ambapo ni kiasi cha shilingi elfu harobaini (40,000) na kueleza kuwa kiasi hicho kitatolewa kulingana na umbali anapo toka Diwani.

Alexanda pia amesema kiasi cha shilingi laki mbili na themanini jambo ambalo baadhi ya Madiwani walio shiriki katika kikao hicho  wamepongeza utendaji kazi wa mkuu huyo wa wilaya  wakati huo Madiwani wa Halmashauri ya Meru  wakikana kuwa walikuwa wakilipwa posho ya kiasi cha shilingi laki Mbili na themanini (280,000)na kueleza kuwa walikua wakilipwa chini ya kiwango hicho.

Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Arumeru  ameeleza kuwa  sababu iliopelekea  kupunguzwa  kwa posho hizo ni kutokana  fedha  nyingi ambazo zimekuwa zikitumiwa na Halmashauri kuwalipa madiwani kiasi cha zaidi ya shilingi milioni mia nane (800)zimekuwa zikitumika kama posho za madiwani kwa mwaka 
Habari na Michael Nanyaro