Update:

27 July 2016

Yanga kupambana hadi dakika mwisho

Baada ya mchezo wa jana kombe la shirikisho Afrika dhidi ya Medeama kocha wa yanga Hans Van Der Pluijm amesema kikosi chake kimebaki na dakika 90 za kupambana ili kujua hatima yake kwenye michuano hiyo


Akizungumza na waandishi wa habari  hizi jana mchana kwa njia ya simu kutoka Ghana, Pluijm alisema kuwa mechi kati ya Yanga na Mo
Bejaia ya Algeria itakayofanyika Agosti 13 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ndiyo itakayotoa taswira ya kusonga mbele katika safari hiyo ya kuwania ubingwa wa Kombe la Shirikisho.
Pluijm alisema matokeo ya mechi hiyo ya tano yataeleza timu zenye nafasi ya kusonga mbele Kundi A na zile zitakazoshuka dimbani kukamilisha ratiba tu.
"Hatima ya Yanga baada ya mechi ya (leo) jana katika mashindano haya, itajulikana kwenye mechi dhidi ya Mo Bejaia," alisema Pluijm na kuongeza;
"Hatuna sababu ya kukata tamaa, bado tunahitaji matokeo mazuri zaidi kwenye michuano hii inayoshirikisha timu nane bora. Mchezo unaofuata tunapaswa kushinda ili kujiweka vizuri kupata moja ya nafasi mbili za juu kwenye mashindano na kucheza nusu fainali."
Baada ya mechi ya jana dhidi ya Medeama, Yanga itarejea nyumbani kuwasubiri Mo Bejaia kabla ya kumaliza dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) watakaowafuata mjini Lubumbashi Agosti 24.