Update:

28 July 2016

Wanasayansi: Maziwa ya mende yana nguvu mara 4 kuliko ya ng'ombe

KIKOSI fulani cha wanasanyansi kimeibuka na utafiti wa ajabu unaowafanya kuamini kuwa maziwa ya mende yatakuwa dili kubwa siku za usoni hata duniani. Swali la wazi ni je, hata kama yakija kuwa dili mjini, utayanywa?

Timu hiyo ya kimataifa ya wanasayansi wa Institute of Stem Cell Biology and Regenerative Medicine, imegundua virutubisho muhimu vya protini kwenye maziwa ya mende mdudu kero usiyempenda kabisa hasa wale wakubwa.


Maziwa hayo yana virutubisho mara nne zaidi ya maziwa ya ng’ombe na wanasayansi wamedai kuwa yanaweza kuwa muhimu katika kuwalisha watu wanaoongezeka duniani siku za usoni. Ingawa mende wengi hawatoi maziwa, mende aina ya Diploptera punctate, wameonekana kutoa utomvu unaoonekana kama maziwa yenye protini yanayotumika kuwalisha watoto wao.
Ukweli kwamba kumbe wadudu nao hutoa maziwa unastaajabisha lakini kilichowashangaza zaidi watafiti ni kuwa maziwa yao yana nguvu mara tatu zaidi ya ile inayopatikana kwenye maziwa ya kifaru.