Update:

01 June 2016

MANENO YA HARMONIZE AJUTA KUWA STAR, ZIJUE HIZI SABABU ZAYEYE KUJUTIA.“Ustaa ni mzigo wa mwiba ukiubeba lazima utaumia” Unakumbuka Rapa Fid Q alishaimba hivyo ok  well hii sio siri kwa watu wengi maarufu ambao waliwahi kutamani kuishi kistaa na sasa wanajutia hali hio.

 WCB staa Harmonize naye ameanza kujutia maisha ya ustaa kupitia ujumbe wake instagram kuhusu mategemeo ya maisha ya umaarufu ni tofauti na alivyowazia.

Kupitia ukurasa wake wa IG unaopatikana kwa  jina la Harmonize_tz  amendika haya Nilikuwa Sijuwi Kuwa Umaarufu Una Mambo Mengi Kiasi Hikii Daaah Sio Rahisi Kuyashinda Peke Yangu M/mungu Simama Nami Hadi Siku Yangu Ya Mwisho Umaarufu Isiwe Sababu Ya Kukukosea Na Kuwakosea Wazazi Wangu Pamoja Na Ndugu Rafiki Pia Nakuomba Unijalie Mwisho Mwema Mimi Na Nduguzangu Woooote Walio Bahatika Kusoma Hapa Tuseme Ameen