Update:

Nguvu ya kuanza sehemu ya IA journey of thousand miles must begin with a single step (Lao Tzu)

Safari ya maili elfu lazima ianze na na  hatua moja

Mara nyingi tumepata
mawazo mazuri kupitia mikutano na taarifa mbali mbali juu ya kuanza biashara fulani, kukamilisha miradi fulani, kuwaona watu fulani ili kufika mbali kiuchumi, kimahusiano na , kiroho

Wengi tumeshindwa kuanza Kwa sababu tunakua na sababu nyingi za kawaida

utaskia mara ooh ningeanza biashara hii sema tatizo ni mtaji. shida si pesa shida ni wazo ulilonalo ambalo bado hata hujaliandika chini. Kwenye uchumi tunasema ‘hakuna mtu mwenye shida ya Fedha bali shida ya mawazo (no body has money problem but an idea) nenda bank watakuambia

Halaf hivi ni kweli hauna mtaji wakati una miliki smart phone na power bank yake?
Hivi ni kweli hauna mtaji wakati wakati kwa wiki muda wako wa maongezi Kwa ajili ya kusocialize ni elfu kumi Kwa wiki ni shiling ngapi Kwa mwez Je na baada ya miezi mitatu je?

Hivi ni kweli hauna mtaji unaalikwa kwenye mikutano yenye mawazo na fursa za biashara unakataa just because Kuna kiingilio cha elf 10?

Hauna mtaji wakati una nguvu na elimu ya degree juu?
Kabati limejaa nguo na viatu Vipya una cheni za silver na dhahabu?

Hauna mtaji wakati una ndugu jamaa na marafiki wenye uwezo wa kukusaidia na ukipewa hela unasema ni ndogo so unaenda kupoza Roho nazo?Utaskia wengine wakisema oh ningeanza lakini nasema upepo Kwanza duuh endelea bana kusoma upepo wengine wanasoma account balance

Wengine hawaanzi kutimiza malengo Kwa sababu wanasubiri mtaji Uwe mkubwa my dear utasubiri sana wengine wanachanja mbuga

Wengine hawaanzi eti Kwa sababu anaona mawazo yake n mapya sana. Laiti ungeleijua ulimwengu umechoshwa na mambo ya kawaida ungeleta Hilo lako Jipya Uwe mkombozi

Wengine hawaanzi vile tu hawapati support kutoka Kwa watu, darling wengine hawajui hata hatma yao ya kwako wataielewa kweli?

Kama unataka kufanikiwa shauku yako ya kuanza lazima iwe kubwa kuliko udhuru za kawaida unazozitoa
(if you want to succeed your desire to start should be greater than your common excuses)

                                                              Just start

Neema Ezekiel Mwaipela 
0754783196
Arise and shine

No comments