Update:

Mume, mke wafa baada ya kula ugali maharage

Wakazi wawili wa kitongoji cha majengo kijiji cha msebehi,wilaya ya uvinza ,mkoa wa kigoma,Edson kahenela,(68)na mke wake Merisiana Petro (56) wamefariki dunia baada ya kula ugali na kwenda kulala,Tukio hilo lakusikitisha limetokea mei 7 mwaka huu


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui, jana alisema kabla ya vifo vya wanandoa hao walikula ugali wa dona la mahindi na maharage kisha wakaenda kulala, lakini hawakuamka hadi miili yao ilipokutwa chumbani asubuhi ya Mei 8, mwaka huu.
Alisema ililibainika kuwa wamekufa baada ya watoto wao kuona hawajaamka kwa muda mrefu tofauti na kawaida yao na kuamua kwenda kutoa taarifa kwa baba yao mdogo Jemes Kahenela kuwa baba na mama ya waliingia ndani kulala lakini hawajaamka.
“Baba yao mdogo alipata mashaka na kufatilia nyumbani kwa marehemu na kuvunja mlango saa 8:30 mchana. Baada ya kuvunja mlango waliwakuta wakiwa wamefariki dunia wakitoa povu mdomoni la rangi ya njano na chanzo cha vifo hivyo bado hakijajulikana,” alisema.
Kamanda Mtui alisema uchunguzi wa tukio hilo la vifo vya mke na mme bado unaendelea ili kubaini chanzo chake.
Wakati huo huo, mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja, Ligwa Mayala, mkazi wa kitongoji cha Kazaroho, wilaya ya
Uvinza, amefariki dunia na mtu mwingine Mayala Zalia (27) kujeruhiwa baada ya nyumba yao kuungua na moto.
Kwa mujibu wa Kamanda Mtui, tukio hilo lilitokea Mei 8, mwaka huu maeneo ya mto Nsima Lugufu.
Alisema chanzo ni upepo mkali kupeperusha cheche za moto kutoka kwenye jiko walilokuwa wanapikia kisha kushika nyumba nzima