Update:

DEGREE/DIPLOMA SIO KAZI .SEHEMU YA TISA

Masomo yaliopita tumeona ya kwamba ujasiriamali ni roho kamili na sio elimu ya darasani tu, elimu ya darasani inakusaidia kufikiria na kuwa na fikra mwongozo za kukuwezesha kufikiria, kupanga na kuamua ktk mazingira ya kisasa. Naam kuna watu wengi pia ambao hawakusoma masomo ya biashara wala kozi za kijasiriamali lakini wapo makini sana na ujasiriamali. Elimu ya darasani inakuandaa kutumikia mifumo ya kibepari na kibeberu ambayo kama ww ni maskini basi unakuwa umeshikilia makali

UJASIRIAMALI UNAJIFUNZA UKIWA NDANI YA UJASIRIAMALI SIO NJE YA UJASIRIAMALI.

Tofauti kubwa iliyopo kati ya Mjasiriamali na mfanyabiashara ni kuwa Mjasiriamali ni champion, Mjasiriamali anaongeza thamani ya bidhaa, anaunda bidhaa, anabuni bidhaa anatengeneza bidhaa na kisha kuziuza au kutafuta wasambazaji

Mfanyabiashara yeye ana nunua na kuuza bidhaa tu zilizoandaliwa na Mjasiriamali.
Uwezekano wa Mjasiriamali kuwa tajiri ni Mkubwa sana kuliko wa mfanyabiashara. Mfano wanaonunua mafuta toka nje na kuleta TZ ni wafanyabiashara lakini, anayesaga ngano na kuuza unga ni Mjasiriamali (Bakhresa mfano)

Sasa utasema kwa nini wajasiriamali wengi hawawi matajiri? Sio kitu automatic kwamba ukiwa mjasiriamali basi ww ni tajiri. Katika America kila mwaka mamilioni ya wamarekani hujiandikisha ktk orodha ya wajasiriamali na kuweka record za uvumbuzi wao, lakini ifikapo miezi mitano tangu kujiorodhesha unakuta ni wachache sana ambao wameweza kugeuza ubunifu huo kuwa bidhaa ya kibiashara (commercial good) na kati ya hao walioweza basi mamia ndio wanakuwa matajiri baada ya muda mfupi.

Huku kwetu sheria za copy wrights sio Kali sana, lakini wagunduzi wengi huishia hata gunduzi zao bila kurekodiwa rasm na serikali, kwa hiyo - invention failure - inakuwa ngumu kukadiria ingawa tunawaona wengi wakianguka.

Kwa hivyo utaona kuwa Mjasiriamali ni jambo tofauti na kuwa mfanyabiashara na pia kuwa mgunduzi ni kitu tofauti na kuwa mwezeshaji (kubadili ugunduzi kuwa bidhaa) kitu kando. na pia unaweza kuwa na bidhaa tayari na usiuzike (marketing skills)

Yaani unakuta kuna steps
•Wazo la bidhaa
•Uundaji wa bidhaa
•Uuzaji wa bidhaa

Wajasiriamali waliofanikiwa ni wale waliokuwa na uwezo wa kumudu mambo hayo yote au walioweza kualika wataalamu wengine kuwasaidia ktk nyanja ambazo hawana utaalamu Nazo.
Mfano microsoft huunda software za computer lakini hardware zinaundwa na Mjasiriamali mwingine.

Ukitengeza bidhaa yako, unaalika wengine kuunda label, kufanya packing, kufanya distribution na kisha kukusanya pesa na kuzifanyia hesabu.

Mjasiriamali kwa ujumla lazima uwe jasiri utake risk na kuzikabili, ujue mambo mengi na au ujue nani Yupo wapi atanisaidia nini.
Sabasaba inakuja tenga siku moja tembelea maonyesho utajua vitu vingi sana.

Ukiwa na ELIMU ya darasani mambo haya yanakuwa rahisi zaidi kuliko yule asiye soma.

Itaendelea......

Na.Adson Kagiye
+255 756 508 071