Update:

Tumia hizi njia 6 kwa kujiongezea kiwango chako cha kujiamini

Ni vibaya sana kujiamini kupita kiasi lakini pia tunatakiwa kuuogopa woga wenyewe na ni heri kujiamini kupita kiasi kuliko kutojiamini kabisa!

Kama leo utaweza kuweka haya mambo 6 kwenye vitendo katika maisha yako ya kila siku utaongeza kujiamini kwa kiwango cha hali ya juu sana!!

1.Wasalimie Wengine kwa tabasamu na waangalie moja kwa moja machoni mwao; Mmarekani anapoongea na wewe huwa anakuangalia machoni moja kwa moja, Mwingereza anakuangalia mwanzoni anapoanza mazungumzo kisha huangalia pembeni anapokaribia kumaliza maelezo lazima akuangalie machoni; Mbongo huwa haangalii mtu machoni, nahisi ndio maana waongo,(lakini sio wote). Kumuangalia mtu machoni kwa tabasamu huuonesha kuwa unajiamini pia hutoa hamasa kwa mtu kukusikiliza na kuamini unachokiongea. Haipendezi kukunja sura sana!!

2.Onesha kukubali sifa na hongera unazopewa na wenzako; Usikatae unapoitwa boss, mkuu, mheshimiwa, ndg, rafiki, dr, prof, tajiri, Mwl, Baba/Mama, Kaka, Dada, pia ukiambiwa shikamoo itikia naona kipindi hamtaki kabisa kuamkiwa!! Shida tunajuwa hamjiamini au muda mwingine mnahisi hamstahili! Kukubali sifa na heshima unayopewa inakusaidia na wewe kumpa mtu mwingine, hivi kama ukisifiwa tu kwa nguo nzuri uliyovaa unakasirika je, utamsifia mwenzio hata kama kanunua gari nzuri? Hii itakufanya ukose kujiamini!!. Wenzako wanajikubali wao hata kabla ya wewe kuwakubali!!

3.Usifanye matatizo yako yakawa ndo mazungumzo yako binafsi! Chukulia maisha yako katika hali ambayo ni chanya! Wote tumewahi kuumia, wengi bado ni maskini na walalahoi but still tunapambana! Usipende kulalamika au kujihukumu hii itakufanya uishi kwenye mambo ya nyuma au mambo ya mbele wakati maisha ni sasa!! Kuna tofauti kubwa kati ya mshindi na mlalamikaji hivyo inabidi usichukulia mambo kiubinafsi sana kwani utashindwa kujiamini mbele za watu! Keep it simple!!

4.Usipende sana wakuchukulie kuwa wewe ni mtu maalumu; Wale wa kujionesha sana!! Usipende kuishi machoni mwa watu muda wote! Hii inaonesha kuwa hutambui thamani yako! Mtu anayejiamini tayari ameshajua heshima na thamani yake kazi yake yeye ni kuilinda tu! Piga chini kupenda kushangiliwa na kupigiwa makofi kila siku IPO siku utajishangilia na kujipigia makofi mwenyewe!

5.Kabiliana na vipindi vigumu kwa kuongeza utendaji wako; "Gari hutumia generator kuchaji battery lake linapokuwa katika mwendo". Unapukuwa katika changamoto ndo muda wa kufanya maajabu ili kumkera adui yako, kumfanya atae machozi au hata akuogope! Majaribu huwa mtaji na hukufanya ujengeke kishujaa na kuishi kwa kujiamini kila siku! "Kama hukutani na vikwazo basi wewe hautafanikiwa kabisa". Simamia changamoto songa mbele!!

6.Chagua kuona makosa na kukatiliwa kama fursa ya kujifunza; Usijikulie kuwa huwezi hata siku moja! Hata ukishindwa hiyo ni nafasi ya wewe kujifunza na jiambie mwenye kuwa unaweza!! Kama unafikiria kuwa huwezi kweli huwezi, na kama unafikiria kuwa unaweza kweli unaweza! Chagua kufikiria kuwa unaweza kwani sisi kile tunachokifikiria na kama huamini kuwa unaweza hutakaa ujiamini hata siku zote!!

"I is better to die standing rather than to live under your knees"(Che Guavara)

Pia kuvaa vizuri kutakufanya ujiamini, uzoefu, kujiandaa mapema kabla ya tukio, na maadili mema hasa ya kidini vyote kwa pamoja vitakupa ujasiri kiasi cha kuogopwa!!
Imeandikwa na Mr.Adson Kagiye :0756 508071

...Life Tips...

No comments