Update:

Onesmo :Mpango wa biashara ni kauli rasmi ya malengo ya biashara

Mpango wa Biashara
Mpango wa biashara ni kauli rasmi ya
malengo ya biashara , sababu zinazoyafanya
yakisiwe kuwa yanawezekana, na mpango wa
kutimiza malengo hayo. Aidha inaweza kuwa
na habari msingi kuhusu shirika au kundi
linalojaribu kufikia malengo hayo.
Malengo ya biashara yanaweza kufafanuliwa
kwa mashirika ambayo lengo lao ni faida na
yale yasiyo ya faida. Mpango wa biashara za
mashirika ya faida kimsingi husistiza malengo
ya kifedha, kama vile faida ama kupata mali.
Ramani za biashara za mashiirka yasiyo ya
faida na yale ya serikali husisitiza zaidi
kwenye azma ya shirika hilo ambayo ndiyo
nguzo ya serikali ama hali yao ya kutotaka
faida ama kutotoza ushuru kwa usanjari huo-
ingawa mashirika yasiyo ya faida yanaweza
pia kuzingatia mapato. Katika mashirika
yasiyo ya faida, matatizo hutokea wakati kuna
juhudi za kusawazisha lengo na "tofauti za
faida" (au mapato). Mipango ya biashara
inaweza kuwa inalenga mabadiliko ya
mitazamo na utambulisho wa wanunuzi,
wateja, walipa kodi ama jamii kwa ujumla.
Mpango wa kibiashara wenye mabadiliko
katika mitazamo na utambulisho kama
malengo yake makuu unaitwa mpango wa
soko .

No comments