Update:

Moja ya mada iliyotelewa katika semina ya ujasiriamali inayoendelea AJTC

TUNZA MUDA WAKO KUONGEZA UFANISI WA KAZI

Watu wengi wanashindwa kuwa na ufanisi kwa sababu ya matumizi mabaya ya muda. Hata hivyo kila binadamu ana masaa 24, siku 7 kila wiki na miezi 12 kwa mwaka. Tafiti za matumizi ya muda zinaonyesha ni watu wachache sana wanatumia nusu ya muda wao wa kazi kuzalisha na kwa
sababu ya matumizi mabaya ya muda wenginge wanakosa hata muda wa familia zao. Ili kutumia muda wako vizuri ni vema ukatambua mambo yafuatayo.

1. Mambo yanayoiba muda wako: Muda unapotea kwenye vitu vingi ambavyo sio vya lazima kwa wakati fulani. Kwa mfano matumizi ya simu yasiokuwa na utaratibu, social media (whatsapp, instragram, face book n.k), watu wanokutembelea
bila taarifa, kukosa mpango wa siku, kushindwa kufanya maamuzi, mikutano isiyo ya lazima, sherehe, kutaka kufanya mambo mengi wakati mmoja, siasa, n.k

2. Ili kuongeza ufanisi katika kutumia muda wako hakikisha

• Panga kazi zako kwa umuhimu (prioritization)- yapo mambo membi ya kufanya lakini chagua yale ya msingi. Kila unapopanga jambo jiulize je ni muhimu? Linaniongezea nini katika biashara, kazi,
familia au jamii yangu?

• Andaa mpango wako wa kazi kila siku (to do
list)- unataka kufanya nini na wakati gani? usikose diary yako au mahali utaandika vitu unataka kufanya. Kila siku jioni panga utafanya nini kesho yake na baada ya kazi tiki mambo uliyofanya na yaliyobaki.

• Jifunze kusema hapana. sifa kubwa ya watu wenye mafanikio ni kusema “hapana”- “ability to say no”. Usifuate mkumbo fanya vitu ulivyopanga.

• Jipangie muda wa emergence na vitu ambavyo hukutarajia muda huu unaweza kuupa asilimia 10 ya muda wako. Mambo mengine yapangie muda kabla.

• panga ajenda ya mikutano yako hata kama unaenda kukutana na mtu uwe na ajenda. Baada ya hapo aga endelea na kazi zako.

• Fanya maamuzi kwa haraka na uwe mtu wa
vitendo “be an action oriented person”. Maneno yasiyokuwa na vitendo ni siasa na hayaleti matokeo. “Ukisema kitu na hukifanyi, tambua
unafanya siasa badala ya kazi”

Na. Adson Kagiye.