Update:

Sister P: Hakuna msanii mwenye kasi kwa sasa ukilinganisha na enzi zetu
Rapa mkongwe wa kike kwenye muziki wa Bongo, Sister P, amesema kwa sasa hakuna msanii mwenye kasi iliyofikia enzi zao ama rapa wa kike mwenye spidi kama alivyokuwa yeye wakati anawika viunga mbalimbali Tanzania.
 http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2016/03/Sister-P-200x194.jpgAkiongea na Mwandishi wa www.Timesfm.co.tz, P ametoa mfano wa rapa Chemical akisema kuna sehemu nyingine hajulikani kwa hiyo hasogei kwa kasi bali anajitahidi.

“Kasi tulikuwa nayo sisi enzi zile, sasa hivi hakuna anayekuja kwa kasi, huyu (Chemical) anajitahidi kasi sio mchezo bado mapengo yetu yapo makubwa sana sasa hivi fake wengi sana, umarekani mwingi mbwembwe mpaka wanaharibu,” alisema.

“Siwezi kuwataja lakini nikisema fake kila mtu anajua, zamani ilikuwa game la muziki sasa hivi ni game la kibiasharam” aliongeza.

Source: Timesfm

No comments