Update:

Ommy Dimpoz Aelezea Uhusiano Wake na Diamond

 

Ommy Dimpoz aliwahi kuwa rafiki mkubwa wa Diamond lakini urafiki wao kwa sasa umeonekana kupungua au haupo kabisa.

Hitmaker huyo wa ‘Achia Body’ ametueleza hali ilivyo sasa.

Amesema hana ukaribu sana na Diamond kwa sasa lakini hana tatizo naye.

“Hapa hakuna mambo ya kufichaficha, kwamba haina noma hata jana nilikuwa naye. Vitu viko wazi vinaonekana hatuko karibu kama zamani, hilo liko wazi. Lakini itakapotokea huko mbele mimi sina tatizo kabisa,” amesema.

Kwa upande mwingine Ommy amedai kuwa anachofanya kwa sasa ni kujikita kwenye mambo yake zaidi.
Source: mwanaharakati mzalendo

No comments