Update:

Fella aeleza kwanini wasanii wakifarakana na mameneja wao hawachukui muda wanapotea


Meneja wa Yamoto Band na TMK Wanaume Family, Mkubwa Fella amedai wasanii wengi hupotea kwenye muziki muda mchache baada ya kuachana na mameneja wao kutokana kushindwa kujisimania.

fella-1
Akizungumza katika kipindi cha Mkasi TV, Fella alisema wasanii wengi wanafeli kutokana kuwa na matumizi mabaya ya pesa wanazozipata.
“Wasanii wakitanzania nikwambie kitu, kwenye kurekodi ndio wanajua labda ninaweza nikamsomesha producer alafu nikawa namlipa taratibu. Lakini ule usumbufu wa kusema kunakupeleka ngoma kwenye radio na TV hawaujui, wao wanajua ikitengenezwa ngoma tu itapigwa, kwa sababu ngoma inapotengenezwa sio mwisho pale,” alisema Fella.
Aliongeza, “So mwisho wa siku labda mimi na Tale hatulali kuvamia radio mbalimbali pamoja na TV , leo radio hii kesho ile, kesho nikikuamsha nakwambia nenda kapige picha kwa Michael ni mimi nimekuforce. Tena kama ameondoka kwa meneja wakati mfuko bado unacheka, mawazo yake ni bata tu sio kazi tena. Kwa hiyo management inakuwa makini kuangalia vitu hivi visitokee,”

No comments