Update:

04 February 2016

Wabunifu chipukizi walivyolipamba jukwaa la Lady In Red Fashion show 2016

DSC_0753
Wabunifu zaidi ya thelasini (30) wameweza kulipamba vilivyo jukwaa la mitindo hapa nchini la Lady In Red fashion show 2016 lililofanyika jijini Dar es Salaam huku likishuhudiwa na wadau mbalimbali wa mitindo hapa nchini.
Jukwaa hilo linaloandaliwa kila mwaka na Mama wa Mitindo nchini,  Asya Idarous Khamsini  ameelezea kuwa lengo la jukwaa hilo ni kuwa kimbilio la wabunifu chipukizi na kama darasa la tasnia hiyo.
Onesho hilo kwa mwaka huu ni la 12 tokea kuanzishwa kwake huku likia limewatoa wabunifu chipukizi mbalimbali hapa nchini ambao wanamajina makubwa kwa sasa.
Mlimbwende akipita mbele ya mashabiki wa vivazi katika onesho la vivazi la Lady in Red  lililofanywa na mwanamitingo nguli Asya Idarous Khamsini kwenye ukumbi wa Danken House siku ya Jumapili January 31, 2016.
Mlimbwende akipita na kivazi mbele ya mashabiki wa mitindo.
Ni Lady in Red chini ya mwanamitindo nguli Asya Idarous Khamsini. (P.T)
Mlimbwende ndani ya kivazi chekundu

Mwanamitindo nguli Asya Idarous Khamsini  akipita kwenye jukwaa kuwashukuru wale waote waliofanikisha oneshohilo kufanyika huku akisindikizwa na Miss Universe
Mwakilishi wa blog ya Vijimambo ambaye ni mmiliki wa Blog ya Pamoja, Geofrey Adroph akipikea cheti kwa niaba ya Vijimambo blog baada ya kutambulika mchano wa blog hii katika masuala mazima ya mitindo.
Baadhi ya wageni waliofika katika onesho la mitindo lililofanyika siku ya jumapili
Hizi picha za chini ni wanamitindo chipukizi wakionesha umahili wao katika mavazi ya aina zote