Update:

06 February 2016

Somalia: Al-Shabab yauteka mji wa Merca

Wanajeshi wa Kenya wakiwa kwenye moja ya kambi yao kukabiliana na wapiganaji wa Al-Shabab
Wanajeshi wa Kenya wakiwa kwenye moja ya kambi yao kukabiliana na wapiganaji wa Al-Shabab

Wapiganaji wa kundi la Al-Shabab wameuteka mji wa Merca, nchini Somalia, bila hata hivyo kumwagika damu baada ya askari wa kikosi cha Umoja wa Afrika (AMISOM) kuondoka katika mji huo.

Mkuu wa jimbo la Shebelle nchini Somalia amethibitisha taarifa hii, akibaini kwamba wapiganaji wa Al-Shabaab wameuteka mji wa Merca baada ya kuondoka kwa vikosi vya Umoja wa Afrika.
Askari wa kikosi cha Umoja wa Afrika (AMISOM) waliondoka tu katika mji huo na wapiganaji wa Al-Shabab wakaingia.
“Mji wa Merca umetekwa bila ya damu kumwagika, amesema Ibrahim Said”,
Vikosi vya Umoja wa Afrika viliwahi kuudhibiti mji huo wa Bandari kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu.
Inaonekana kuwa kupotea kwa mji wa Merca kutoka mikononi mwa askari wa Umoja wa Afrika na wale waanounga mkono Serikali dhaifu ya Somalia ni pigo kubwa kwa Serikali na kikosi cha Umoja wa Afrika (AMISOM), baada ya kuanzisha vita dhidi ya Al-Shabab kwa zaidi ya miaka kumi sasa.