Update:

Nilikuwa nalisoma gemu-Mike TeeMike tee mnyalu 
Mkongwe wa Muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Mike Mwakatundu ‘Mike Tee’.
Mkongwe wa Muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Mike Mwakatundu ‘Mike Tee’ amesema alikuwa kimya kwa muda mrefu kwa vile alikuwa analisoma upya gemu kwani kuna mabadiliko makubwa katika tasnia hiyo kwa sasa.
Alisema fleva za sasa zimebadilika hivyo ni jambo zuri kwa msanii kulifahamu vyema soko la muziki linataka nini na ili iwe hivyo, yampasa kurudi nyuma, kukaa kimya na kuwasoma mashabiki ili kujua wanahitaji nini toka kwake kabla ya kutoa kazi.
“Mimi nawakilisha watu wawili, Mike Tee msanii na Mike Mwakatundu kama taasisi, ilifika sehemu Mike Mwakatundu ilibidi naye apewe nafasi maana ni baba wa watoto wawili (Michael and Michelle) na ni baba wa familia so kuna mambo ilibidi kuyaweka sawa ya kifamilia ili niweze kujigawa vizuri upande wa muziki na maisha ya kawaida,” alisema Mike Tee ambaye amerejea kwa kishondo na kibao chake cha Kiduchu