Update:

21 February 2016

La Liga :Ubingwa Real Madrid ni Ndoto

 

Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane
Klabu ya soka ya Real Madrid kwa mara nyingine tena imetoshana nguvu na Malaga kufuatia sare ya 1-1 katika mchezo uliopigwa jana na kupelekea kuwa pointi 9 nyuma ya mahasimu wao Barcelona ambao walishinda dhidi La Palmas bao ya 2-1.
Huku kocha zinedine Zidane akiwa na kikosi kilichokuwa na upungufu wa Karim Benzema na Gareth Bale akimuanzisha Cristiano Ronaldo ambaye ndiye aliyeifungia bao Madrid dakika 33.
Dakika 2 baadaye Madrid wakapata penati ambayo Cristinao Ronaldo akaipoteza baada ya kuokolewa na kipa wa Malaga – Carlos Idriss Kameni.
Dakika ya 66, Raul Albentosa aliisawazishia Malaga kwa assist nzuri ya beki wa kati Welington na kuufanya mchezo usomeke kwa matokeo wa ba 1-1 hadi mwisho wa mchezo.
Hii inakuwa penati ya 7 kwa Ronaldo kukosa msimu huu,ikiwa ni idadi sawa na mpinzani wake Lionel Messi.