Update:

02 February 2016

Je unaelewa jinsi uchaguzi wa Marekani unavyoendeshwa ?


 
Mwongozo wa kumteua muaniaji urais nchini Marekani Mwongozo wa kumteua muaniaji urais nchini MarekaniMuhtasari:
Kabla ya Wamarekani kuamua nani wanayemtaka awe rais ajaye, wao kwanza huteua nani atakayewania kiti hicho.
Mchakato huo hungo'oa nanga kwa mchujo wa kamati za wajumbe ambapo wananchi hupata fursa ya kumchagua muaniaji kiti cha urais kwa tikiti ya chama cha Democratic au kile cha Republican.
Huu hapa ni mwongozo wa mchakato wa kuteua wagombea.
Je mchakato wa kuteua wagombea huwa vipi ?
Mwongozo wa kumteua muaniaji urais nchini Marekani
Kura za mchujo na mfululizo wa uchaguzi wa kamati za wabunge hufanyika katika kila jimbo na wilaya nje ya nchi ambayo huamua nani atapeperusha bendera ya kila chama.
Mshindi wa mchujo huo anawakusanya wajumbe - hawa ni wanachama wenye nguvu ya kupiga kura kumchagua mgombea katika mikutano ya chama.
Katika makongamano hayo ndipo mgombea wa urais wa kila chama huchaguliwa.
Nini tofauti kati ya kongamano la Chama na mchujo wa mashinani ?Kongamano la chama kinahusisha wanachama wanaokusanyika katika shule, nyumba za watu binafsi na majengo ya umma kujadili wagombea sera zao na mapendekezo yao
na mara nyingi wao hupiga kura waziwazi kwa kuonyesha mikono.
Hata hivyo katika mchujo wa mashinani wajumbe wa chama cha kisiasa huketi wakajadili sera na mapendekezo ya wagombea na huchagua mgombea wao kwa kupiga kura kwa siri wakitumia sanduku la kura.
Kura za mchujo wa mashinani huandaliwa na serikali ilihali kongamano la chama huandaliwa na watu binafsi vigogo wa chama, wanachama kwa jumla.
Kuna aina mbalimbali za mchujo na sheria mbalimbali:• Mchujo wa wazi -"Open":
Mjadala wa kuwania tikiti ya Republican ulifanyika katika jimbo la Iowa
Mchujo huu ni wazi kwa kila mtu mwenye kadi ya kupigia kura bila kujali msimamo wa chama.
Hii inamaanisha kuwa japo mtu anaweza kuwa mwanachama wa Republican anaweza kushiriki katika kura za Demcrats.
Kinyume chake pia ni sawa na halali.
• " Mchujo Nusu wazi: - "Semi" :Hapa wajumbe wanaoruhusiwa kushiriki katika mchujo na upigaji kura sharti wawe ni wanachama waliosajiliwa rasmi katika chama kinachoendesha uchaguzi huo wa mchujo.
Kwa Mfano wanachama wa chama cha Democrat pekee ndio wanaoruhusiwa kushiriki katika mchujo huo wa kumchagua muaniaji tikiti ya urais kwa chama cha Democratic.
Hata hivyo kwa wale wapiga kura ''Huru/Binafsi''ambao hawaegemei upande wowote ima ni Democrat ama Republican wanaweza kushiriki katika mchujo huu.
Jimbo la New Hampshire huwa linaendesha mchujo nusu .
• Mchujo Uliofungwa - "Closed" :Hapa wajumbe wa chama waliojiandikisha kikamilifu ndio wanaoruhusiwa kupiga kura katika majimbo waliojiandikisha pekee.
Kila mjumbe anaipigia chama chake kura kumchagua muaniaji tikiti wa chama hicho.
Kura za mchujo zinatofautiana katika kila jimbo.
Katika majimbo mengine,wajumbe wa chama cha Democratic huruhusiwa kukiri wazi wazi kuwa wanampendelea mgombea mmoja dhidi ya mwengine.
Hata hivyo katika chama cha Republican mambo huwa ni ya siri.
Mgombea urais wa Republican Ted Cruz ametumia muda mwingi katika kampeni Iowa
Wajumbe ni nani?Michujo na kamati za wajunbe hazina uwezo wa kumchagua moja kwa moja mgombea urais.
Hiyo kirasmi na shughuli na jukumu la wajumbe katika mikutano ya vyama .
Wajumbe ni wanachama wa vyama mbalimbali, hivyo wanauwezo wa kumpigia kura muaniaji kiti cha urais kuambatana na matakwa ya wanachama walioshiriki katika mchujo.
Wakati mwengine inawezekana kwamba mgombea hakuweza kupata wajumbe wa kutosha kushinda uteuzi wa chama hicho,na ikifikia hapo basi makubaliano mahsusi kati ya wagombea ndio huamua yupi kati ya washindani wakuu anayechaguliwa kupeperusha bendera ya chama katika uchaguzi mkuu.
Mapatanisho na mazungumzo kati ya mawakala wa wagombea wakuu na hata wakati mwengine raundi ya pili na hata ya tatu ya kura miongoni mwa wajumbe wa chama huishia kwa mgombea mmoja.
Si aghalabu wakati mwengine kumpata muaniaji mkuu hata kwenye kura za mchujo hususan pale anapoibuka maarufu mgombea mmoja dhidi ya wenzake mapema katika mchakato huo wa uteuzi.
Hilo likitokea wagombea wenza hujiondoa mapema na kutumia muda wao mwingi kuwapatanisha wafuasi hasidi kwa manufaa ya chama kabla ya uchaguzi mkuu.
Kwa nini Iowa na New Hampshire hupiga kura wa kwanza ?Hakuna sababu hasa -
Mwaka huu 2016 Kamati za Wajumbe maalum katika jimbo la Iowa watamchagua muaniji kiti cha urais katika chama chao tarehe 1 Februari.
New Hampshire kwa upande waowatashiriki wajibu huo wao wa kikatiba tarehe 9 Februari.
Wahakiki wanadai nchi majimbo hayo mawili hayastahili ushawishi walionayo kwa sababu matokeo hayo si wakilishi kwa idadi kubwa ya wamarekani.
Kwa mfano, Iowa na New Hampshire ni majimbo madogo mno na yanawakilisha haswa maeneo nje ya mijini ambapo idadi ya wazungu ni asilimia 94% ikilinganishwa na asilimia 77 % ya idadi ya wazungu kwa mujibu wa takwimu ya taifa ya.
Mgombeaji wa tikiti ya Republican Donald Trump ameimarika sana katika kura za maoni
Hata hivyo majimbo hayo mawili yanajipigia debe yakisema kuwa asilimia kubwa ya wapiga kura wao ni wasomi katika maswala ya siasa na wanauweza na tajriba ya kuwawajibisha wagombea mbali na kuhoji sera zao na mashiko yao
Je mgombeaji akiibuka mshindi katika majimbo ya Iowa au New Hampshire huwa ndiye atakaye pigiwa upatu kuwa muaniaji mteule wa chama ?Si Kweli -
Sio daima kuwa muaniaji kiti cha urais wa chama anayeibuka mshindi katika kongamano la wajumbe katika jimbo la Iowa , ndiye atakayeibuka kuwa muaniaji mteule wa chama.
Hata hivyo muaniaji mteule huko Iowa huibuka na ari ya kuendelea kuwashawishi wajumbe katika majimbo mengine na mara nyingi huwa wanashawishika.
kwa kweli Iowa husaidia kuimarisha ama hata kuvunja ndoto za wawaniaji wengi wa tikiti cha urais katika vyama vyao.
Licha ya kutamba kwenye mijadala mgombeaji wa tikiti ya Democratic Martin O'Malley ameshindwa kusisimua wapiga kura
Wahakiki wanasema kuwa kwa sababu New Hampshire ndio uchaguzi wa pili na mara nyingi hupewa nafasi kubwa katika vyombo vya habari mshindi huko New Hampshire bila shaka anapata muamko mzaidi wa kujibidiisha na kuamini kuwa anaweza kuibuka mshindi wa chama chake.
Vilevile anayeshinda New Hampshire huwa anaendelea kuvutia hisia za wamarekani wengi haswa wale ambao hawakuwa wameamua watamchagua nani wakati wa awali wa kinyang'anyiro hicho cha uteuzi.
Mwandishi wa BBC Katty Kay anasema: "wagombea wanaoibuka na ushindi katika majimbo ya Iowa na New Hampshire huwa wanajenga hisia ya kasi na kwa hiyo huendeleza kasi kampeni yao bila shaka wakiangaziwa zaidi na vyombo vya habari kuliko ilvyokuwa kabla ya ushindi huo.
"Ukishinda Iowa bila shaka utakuwa kwote kwenye televisheni.
''Kisha kuna fedha na Ufadhili- mgombea anapotwaa majimbo hayo mapema, huwa anafungua milango ya ufadhili kutoka kwa wahisani ambao awali walikuwa hawajui wamdhamini nani.''
''Ni ukweli usiopingika kuwa watu wanampenda mshindi ''kila mmoja wetui anapenda mafanikio''.
Licha ya kuongoza katika kura za maoni bi Hilary Clinton alishindwa mwaka wa 2008 na rais Barack Obama
Jumanne kuu ni nini?Jumanne kuu ni siku ambayo majimbo mengi huandaa michujo au kamati za wajumbe kwa wakati mmoja.
Mwezi Februari 2008, majimbo 24 yalishiriki katika "Super-Duper Tuesday ", Katika mwaka 2012 ni majimbo 10 pekee yalioshiriki katika jumanne kuu.
Mwaka huu, Jumanne kuu imeratibiwa kuwa tarehe 1 Machi.
Majimbo 16 yataandaa mchujo na chaguzi katika majimbo 13 ya Marekani.
Kutaadaliwa uchaguzi katika himaya za Marekani .
Seneta Bernie Sanders ni mshindani wa karibu zaidi wa bi Hillary Clinton katika kinyang'anyiro cha tikiti ya chama cha Democratic
Nini hufanyika baadaye?
Kamati za wajumbe na michujo itaendelea mpaka majira ya joto, na kisha uteuzi wa waniaji kiti cha urais wa vyama utaidhinishwa rasmi katika mkutano ya kitaifa ya vyama inayoratibiwa kufanyika mwezi wa Julai.
Majimbo yote ya Marekani yatatuma idadi mbalimbali ya wajumbe kuwawakilisha kulingana na ukubwa na rekodi yake ya upigaji kura .
Mgombea lazima ashinde kwa wingi wa kura za wajumbe.
Mshindi sharti apate uungwaji mkono na nusu ya wajumbe na zaidi ili kupata uteuzi wa chama hicho.
Muaniaji kiti cha urais kwa tikiti ya Republican anahitaji kura 1236 za wajumbe iliatangazwe mshindi.
Wakati huohuo muaniaji tikiti ya chama cha Democratic anastahili kutia kibindoni kura 2383 iliajihakikishie kupeperusha bendera ya chama chake katika uchaguzi mkuu ujao.