Update:

03 February 2016

Izzo apanga kufuata nyayo za Joh Makini, Diamond


izo1 
MKALI wa Hip Hop Bongo, Emmanuel Simwinga ‘Izzo Bizness

MKALI wa Hip Hop Bongo, Emmanuel Simwinga ‘Izzo Bizness’ ametamka kuwa anajipanga kuhakikisha muziki wake unapiga hatua na kutoboa katika soko la kimataifa kama ilivyo kwa wasanii wengine, Joh Makini na Diamond ambao wamekuwa wakisumbua katika anga hizo.
Izzo Bizness kwa sasa ngoma yake ya Shem Lake aliowashirikisha Mwana FA na G Nako, inabamba vilivyo katika vituo mbalimbali nchini tangu auachie takribani mwezi mmoja sasa.
Akizungumza na Mikito Jumatano, staa huyo alisema kwa sasa maandalizi ya kuhakikisha muziki wake unapiga hatua yanaendelea vizuri japo ni mapema sana kuanza kuzungumzia juu ya suala hilo.
“Nipo katika mipango ya kufanya muziki wangu upige hatua na kwenda kimataifa kama ilivyo kwa wasanii wengine wa Bongo ambapo mikakati hiyo inaendelea japo ni mapema kuizungumzia kwa sasa.
“Lakini tayari nimeshafanya nyimbo kadhaa na baadhi ya wasanii wa nje akiwemo Navio wa Uganda ambaye nilifanya naye wimbo ambao tumeutoa tu ‘online’ kama zawadi kwa mashabiki,”alisema Biznes.