Update:

Waanglikana waunga mkono ndoa za jinsia moja


 
Justin Welby
Waumini wengi wa Kianglikana nchini Uingereza wanaunga mkono ndoa za wapenzi wa jinsia moja ,kulingana na kura ya maoni.
Kati ya zaidi ya waanglikana 1,500 waliohojiwa asilimia 45 ilisema kuwa ndoa za wapenzi wa jinsia moja zinafaa kuendelea huku asilimia 37 ikisema kuwa ni makosa.
Kura hiyo ya maamuzi ya Yougov pia imesema kuwa kuna ongezeko la waumini wa kanisa hilo wanaounga ndoa za jinsia moja katika kipindi cha miaka mitatu iliopia.
 
Anglikana
Msimamo rasmi wa kanisa la Uingereza ni kwamba ndoa inaweza kuwa ya mume na mke pekee.
Miaka mitatu iliopita,kura kama hiyo ya Yougov ilibaini kwamba asilimia 38 ya Waanglikana wanaunga mkono ndoa hizo huku asilimia 47 wakipinga.
 
 Kanisa Anglikana barani Afrika
Katika kura hiyo ya maoni,uungwaji mkono ulikuwa juu miongoni mwa vijana huku ikiwa wale walio chini ya umri wa miaka 55 wakiamini kwamba ni sawa na asilimia 72 wa wale walio kati ya umri wa miaka 25-34, pia wakiunga mkono.
chanzo:bbc