Update:

TFDA walivyonasa mzigo wa magendo ulioingizwa kwenye mpaka wa Namanga Arusha..
Kumekuwa na stori kuhusu ishu Mamlaka ya Dawa na Chakula, TFDA kuingia kwenye kona mbalimbali za Tanzania na kukamata vipodozi vyenye viambata vya sumu pamoja na vile ambavyo vimepigwa marufuku.Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kanda ya kaskazini, Damasi Matiko ametusogezea ripoti jinsi ambavyo walinasa vipodozi hivyo Arusha >>> ‘Dawa hizo zilikamatwa katika gari zikiingizwa katika mpaka wa Namanga… zilikuwa carton zaidi ya 100 na hazikuwa na nyaraka, wenye gari wameukana mazigo huo wenye thamani ya milioni 34‘.


Kingine ni hiki kuhusu athari za vipodozi hivyo vyenye viambata vya sumu >>> ‘Hizi ni bidhaa zisizofaa, mtu atakayetumia atapata madhara kwenye ini, figo.. mwanamke inaweza kumuathiri mfumo wa uzazi na anaweza kuzaa mtoto mwenye mtindio wa ubongo‘- Meneja TFDA Kaskazini, Damasi Matiko.