Update:

Samatta atambulishwa rasmi Genk Ubelgiji


Samatta
Samatta amekuwa akichezea TP Mazembe ya DR Congo
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta ametambulishwa kama mchezaji mpya wa klabu ya Genk ya Ubelgiji.
Samatta amejiunga na klabu hiyo inayocheza Ligi Kuu ya Ubelgiji kutoka kwa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Samatta, aliyetawazwa mchezaji bora wa mwaka Afrika 2015 kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani, ametia saini mkataba wa hadi mwisho wa msimu wa 2019/2020.
  • Samatta, kijana anayevumisha soka ya Tanzania
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, ambaye pia hucheza kama winga, alishinda vikombe sita vikubwa akiwa na TP Mazembe, ikiwa ni pamoja na kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Afrika mwaka 2015.
Ameichezea timu ya taifa mara 20 na kufunga magoli saba.
Samatta
Samatta alitawazwa mchezaji bora wa ligi za ndani Afrika 2015
Akiandika kwenye akaunti yake ya Twitter, Samatta alisema: “Nimejiunga rasmi na <span >@KRCGenkofficial. Nasubiri kwa hamu kipindi hiki kipya maishani mwangu.”