Update:

30 January 2016

Matangazo ya bunduki yapigwa marufuku Facebook

Bunduki
Kundi moja limesema bunduki zilizonunuliwa kupitia Facebook zimetumiwa kutekeleza uhalifu
Watu binafsi hawataruhusiwa tena kuweka matangazo ya kuuza bunduki katika Facebook na Instagram, kampuni ya Facebook ambayo pia inamiliki Instagram imetangaza.
Facebook tayari ilikuwa imepiga marufuku uuzaji wa bunduki bila mtu kuchunguzwa historia yake, lakini sheria mpya sasa zinalenga kuzuia uuzaji na ununuzi wa bunduki kati ya watu binafsi katika mitandao hiyo ya kijamii.
Watu wanaomiliki biashara hata hivyo bado wanaweza kutangaza bunduki zao wakitumia kampuni au mashirika yao kwenye Facebook na Instagram.
  • Obama atokwa na machozi akizungumzia silaha
Mabadiliko hayo yamejiri wiki tatu baada ya Rais wa Marekani Barack Obama kufanyia mabadiliko sheria za uuzaji wa silaha.
Miongoni mwa mengine, Bw Obama ameifanya lazima kwa wauzaji wote wa silaha kuchunguza watu wanaotaka kununua silaha.
Majimbo pia yatatakiwa kutoa habari kuhusu watu ambao hawaruhusiwi kununua silaha kutokana na kutokuwa na akili timamu au kuhusika katika visa vya ghasia.