Update:

15 January 2016

Ebola imerudi tena Sierra Leone..huu ndio uthibitisho wa maofisa afya!!

Jana shirika la Afya duniani WHO lilitangaza kumalizika kwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola huko Sierra Leone.

Headlines zimerudi tena nchini humo baada ya maofisa wa afya kudhibitisha ugonjwa huo kurudi tena na kuua mtu mmoja.

Mwili wa mtu huyo ulipimwa na wataalam wa afya kutoka Uingereza na kuthibitika alikuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola.

Maofisa wa afya wameanza kutafuta watu wote ambao walikutana na mtu huyo kabla hajafariki.

Sierra Leone ni miongoni mwa chini za Afrika Magharibi zilizpkumbwa na ugonjwa wa Ebola uliosababisha vifo vya watu wengi.