Update:

Chelsea wampata Pato kutoka Corinthians


Alexandre Pato
Pato amechezea timu ya taifa ya Brazil mara 27
Chelsea imemchukua mshambuliaji wa Brazil Alexandre Pato kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.
Mshambuliaji huyo wa umri wa miaka 26 ambaye amekuwa akichezea klabu ya Corinthians ya Ugiriki amechezea taifa lake mechi 27 na kuwafungia mabao 10.
Alichezea Brazil katika Michezo ya Olimpiki mwaka 2008 na 2012.
“Nina furaha sana kujiunga na Chelsea,” alisema Pato baada ya kujiunga na klabu hiyo ya Stamford Bridge. “Ni klabu niliyoitamani sana, na nasubiri kwa hamu kuwafahamu wachezaji wenzangu wapya na kucheza nao pia.
"Naishukuru Chelsea kwa kuniunga mkono na natumaini nitawafanyia hisani kwa sababu ya kuwa na Imani name.”
The Blues, walioshinda Ligi ya Premia msimu uliopita, wametatizika sana msimu huu na wamo nambari 13 ligini, ingawa bado wanacheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Kaimu meneja Guus Hiddink amesema licha ya hali kwamba Pato ametatizwa sana na majeraha, hadhani kwamba kumchukua ni kucheza bahati nasibu.
"Si kubahatisha. Kuja kwake hapa kwa mkopo kunatuwezesha kumfuatilia na kujua iwapo anaweza kuzoea ligi hii,” amesema Hiddink.
Chelsea pia wanakaribia kumnunua difenda wa New York Red Bulls Matt Miazga, 20.