Update:

Ubelgiji yahofia kushambuliwa


Washukiwa
Washukiwa wawili wanaotuhumiwa kupanga mashambulio ya mkesha wa Mwaka Mpya walikamatwa wiki hii
Ubelgiji imesitisha sherehe za kijadi za kuwasha fataki mjini Brussels katika mkesha wa mwaka mpya, kwa hofu ya shambulizi.
Meya wa mji wa Brussels, Yvan Mayeur, amesema uamuzi huo umechukuliwa baada ya kufanywa kwa tathmini.
Mwanzoni mwa wiki hii, watu wawili walikamatwa nchini humo kwa kushukiwa kutaka kupanga shambulizi mjini Brussels katika mkesha wa mwaka mpya.
Ubelgiji imekuwa katika tahadhari ya hali ya juu tangu kutokea kwa shambulizi la kigaidi nchini Paris mwezi uliopita.
Baadhi ya wanaoshukiwa kuhusika na shambulizi hilo wapo nchini Ubelgiji.