Update:

Kipindupindu chaua 21 MwanzaMganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Rwakyendela Onesmo

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Rwakyendela Onesmo amesema leo kuwa ugonjwa huo umeenea kwenye maeneo ambayo hayana usafi wa kutosha na vyoo vya kisasa.

 Watu 21 wamefariki dunia na wengine 670 kulazwa katika kambi mbalimbali kutokana na kuugua kipindupindu tangu kilichoibuka mkoani Mwanza Septemba.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Rwakyendela Onesmo amesema leo kuwa ugonjwa huo umeenea kwenye maeneo ambayo hayana usafi wa kutosha na vyoo vya kisasa.

“Ugonjwa huo ni hatari unaambukizwa kwa kula chakula au kinywanji chenye vimelea vya Vibrio cholera, ambavyo husababisha kipindupindu.“Vimelea hivi hupatikana kwenye kinyesi na matapishi ya mgonjwa wa kipindupindu,” amesema Dk Onesmo.

Alizitaja wilaya zilizoripotiwa kuwa na kipindupindu kuwa ni Sengerema wagonjwa 223, ukerewe 263, Ilemela 249 na Magu 10.

Amesema watu waishio katika makazi holela wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa wa kipindupindu kutokana na kutokuwa na vyoo bora na vya kisasa.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga amesema: “Nawaomba wakazi wa Nyamagana kuwa waangalifu, pia mjitokeze kufanya usafi katika maeneo mnayoishi ili kuweza kuondokana na ugonjwa huo.”