Update:

TATIZO LA KUTOPATA RAHA WAKATI WA TENDO LA NDOAhttps://encrypted-tbn0.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcTPxu_qqnuERMXGjQ1VbK2vEK0nWyQ55xmuELcCdgziGoJs2h2x


Wapo ambao wakati wanapofanya mapenzi badala ya kupata raha, husikia maumivu, mwanaume katika uume lakini ni mara chache sana kulinganisha na wanawake. Mwanamke ndiye husumbuliwa zaidi na tatizo hili.
Mwanamke anaweza kukosa raha kabisa na matokeo yake kuumia wakati tendo linapoanza pale mwanzoni ukeni au kwa ndani zaidi. Maumivu haya pia yanaweza kugawanyika katika makundi mawili. Kwanza ni maumivu wakati wa tendo ambayo ndiyo hayo tuliyoyaona hapo juu na maumivu baada ya tendo.


Kuumia wakati wa tendo
Maumivu haya hutokea pale uume unapoanza kuingia ukeni na hutokana na uke kuwa mkavu.
Hili linaweza kusababishwa na maandalizi duni kabla ya tendo, matatizo katika mfumo wa homoni au kupoteza msisimko na hamu ya tendo.

Kubana kwa misuli ya uke pia huchangia ingawa tatizo hili zaidi ni la kisaikolojia kutokana na mwanamke kuwa na woga wakati wa tendo.

Kuwa na makovu ukeni kutokana na athari za kukeketwa, uwepo wa michubuko na vidonda au maambukizi ukeni mfano fangasi ya muda mrefu na maambukizi mengine hasa magonjwa ya ngono.
Uvimbe ukeni au uwepo wa jipu na vipele, kuumia kwa kufanyiwa vipimo au baada ya kuzaa kwa njia ya kawaida endapo hukupona vizuri.

Kuhisi maumivu baada ya tendo
Maumivu haya hutokea muda mfupi baada ya tendo la ndoa. Mwanamke huhisi maumivu kwa ndani zaidi ukeni au chini ya tumbo. Maumivu huwa makali na huchukua muda mrefu.
Maumivu ya chini na ndani zaidi ukeni huleta hisia kama muwasho mkali wa pilipili au kama unakatwakatwa na viwembe na ukinawa unazidi kupata maumivu.

Maumivu ya ndani zaidi ukeni wakati mwingine huambatana na hali ya kuhisi kama kuna kitu kinasukumwa wakati wa tendo na unapomaliza tendo ukinawa unahisi kitu kimevimba ndani ukeni kama kigololi. Maumivu huwa chini ya tumbo na wakati mwingine husambaa kulia na kushoto ya mirija. Wengine huumwa na kiuno hata kutembea inakuwa shida mara tu baada ya kumaliza tendo.

Hali ikiwa mbaya mwanamke hutokwa na damu baada ya tendo, hali ambayo siyo dalili nzuri kwani hata saratani ya shingo ya uzazi nayo huonyesha dalili hii ya damu.

Hali ya maumivu pia huambatana na kutokwa na majimaji ukeni wakati mwingine yakiambatana na muwasho mkali na harufu. Hata wanaume wanaweza kutokwa na damu baada ya tendo badala ya manii.

Nini cha kufanya?
Tatizo hili ni kubwa na lina vyanzo vingi kama tulivyoona, hivyo ni vema kufanya uchunguzi kujua chanzo halisi ndiyo tiba ifuate.

Epuka kutumia dawa bila ya kujua chanzo halisi.
Uchunguzi hufanyika katika hospitali za mikoa, wilaya kwa madaktari wa magonjwa ya kinamama.
Ni vema uwahi hospitali.