Update:

Mgombea Urais Edward Lowassa alivyosindikizwa kurudisha Fomu za kugombea Urais 2015 katika ofisi za NEC…
Mgombea Uraisi pamoja na mgombea mwenza kupitia UKAWA akiojiwa na wanahabari wa vyombo mbalimbali vya Habari

Edward Lowassa akitoka kwenye Ofisi za Tume ya Uchaguzi baada ya Fomu zake kupokelewa. , huku akiwa na baadhi ya Viongozi wa UKAWA

August 21 2015 ndio siku ambayo Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania NEC ilitangaza kwamba Wagombea wote wa Urais wanatakiwa kurudisha Fomu zao Makao Makuu ya Ofisi za Tume hiyo, Posta Dar es Salaam Tanzania.

Wagombea wa Urais kutoka kwenye vyama mbalimbali vya siasa wanaendelea kurudisha Fomu hizo, hapa ninazo pichaz ambazo nimekusogezea baadhi ya picha uone jinsi mgombea wa Urais kupitia CHADEMA na UKAWA, Edward Lowassa alivyorejesha Fomu zake huku akiwa ameongozana na baadhi ya Viongozi wa UKAWA pamoja na wanachama.
.


Kuna Magazeti ya Tanzania August 21 2015 yameandika kwamba Fomu zinarudishwa kimyakimya, ni kwamba Tume ya Uchaguzi ilitoa maagizo kwamba hakutaruhusiwa kuwa na mbwembwe zozote wakati wa urudishwaji wa Fomu hizo na pia Wagombea wanatakiwa kusindikizwa na watu wachache kabisa ili kila kitu kifanyike kwa haraka kwa sababu Vyama vyote vinarudisha Fomu siku moja tu ambayo ndio leo na mwisho ni saa kumi jioni.A