Update:

Mapunye na athari zake kwa ngozi yako
Mapunye ni aina ya magonjwa ambayo hushambulia zaidi sehemu ya kichwani mwa binadamu kama ambavyo tulinavyoona watu wengi wakiangaika sana.

Ni pamoja na; Kutumia vifaa vya nywele kama chanuo la kuchania nywele kwa zaidi ya mtu mmoja hususani pale ambapo mmoja wa watumiaji hao ana maambukizi ya vimelea vya fangasi hao.
-Kugusana na mtu aliye na maambukizi tayari -Kushirikiana mavazi aina ya kofia na mtu aliyekwisha pata maambukizi hayo


Ni nani yuko hatarini?
Watu ambao huweza kupata maambukizi ya mapunye ni wafuatao:
-Wale wanaoshirikiana na wenzao vifaa vya kunyolea bila kuvisafisha vizuri
-Wanaoshirikiana vifaa vya kufanya usafi wa mwili zikiwamo taulo
-Wanaotoka jasho hasa kichwani kwani huweza kuweka mazingira mazuri zaidi kuruhusu maambukizi yatokee kirahisi
-Wanaofanya kazi zinazohusisha uwekaji vichwa kwenye maji yaliyotuama kwa muda mrefu
-Wale ambao tayari wana fangasi za kichwani kwani ni rahisi kwa fangasi hao kujirudia.
-Wanaofanya usafi wa mwili kwa kutumia maji yaliyobeba vimelea
-Wasiojikausha vichwa baada ya kuoga au kufanya usafi wa kichwa
-Watu wenye maradhi yanayosababisha kushuka kwa kingaikiwamo kisukari.
-Wale wanaokunywa dawa za kuua vimelea (antibayotiki) kwa muda mrefu
-Watoto wadogo ambao hawajafikia umri wa balehe.

Jinsi ya kuyatambua
Mara nyingi aina hii ya fangasi hugundulika kwa macho hasa kwenye maeneo ambayo fangasi hao wapo kwa wingi. Kwa kutazama ngozi ya sehemu ya kichwa iliyoathirika na maambukizi ya fangasi hao, utaweza kuona madhara yanayokukabili.


Kwenye uhitaji wa vipimo basi sehemu ya ngozi iliyoathirika huchukuliwa kwa ajili ya kufanya vipimo vya maabara na kuangalia aina sahihi ya fangasi
Matibabu
Mara nyingi mapunye hutibika kwa dawa za kutibu fangasi za kupaka ambazo hutibu mapunye na kuyaponyesha kabisa bila kuhitaji kutumia dawa za kumeza. Hii ni kwa kuwa ni rahisi kwa dawa ya kupaka kupenya kwenye ngozi na kusababisha matokeo yanayohitajika.

Matibabu ya mapunye huchukua muda mfupi kuonyesha matokeo mazuri
Kama nilivyoandika kwenye makala zilizopita matibabu kuwa magonjwa huwa yanawezekana kutibika mkombozi sanitarium clinic nakuyamaliza kabisa

Kwa sababu hiyo, ni vizuri kwa mgonjwa wa fangasi kutumia dawa mpaka wiki mbili baada ya dalili za maradhi kutoweka.

Jinsi ya kujikinga
Kuna mbinu mbalimbali za kujilinda usipatwe na fangasi:
-Hakikisha mwili wako hasa kichwani yanabaki na ukavu muda wote
-Osha nguo, taulo na mashuka kuhakikisha fangasi wanaondolewa
-Epuka kushirikiana vifaa vya kunyolea nywele hasa kama hakuna namna ya kuvisafisha na dawa maalum ya kuua vimelea kabla hujatumia

-Epuka kushirikiana katika utumiaji wa vifaa vya kufanya usafi wa mwili kama mataulo. Kama kazi yako inahusisha ukaaji wa muda mrefu kwenye maji basi hakikisha unakausha mwili hasa sehemu za kichwa au uweke dawa ya kuzuia fangasi kwenye maji hayo.