Update:

19 March 2018

March 19, 2018

GESI YALETA KIZAAZAA, WATU WATANO WANUSURIKA KIFO KIDONGO CHEKUNDU - RPC SHANNA

WATU watano wamenusurika kifo baada ya nyumba kuteketea kwa moto, katika kitongoji cha Kidongo Chekundu kata ya Magomeni wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani. Hili ni tukio la pili linalohusiana na janga la moto kutokea ndani ya wiki moja mkoani hapo ambapo machi 11, nyumba ya Makulata Petro iliungua huko Magwila wilaya ya Chalinze na kusababisha vifo vya watu wanne na majeruhi wawili .

Kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Jonathan Shanna alielezea tukio hilo, limetokea machi 18 saa 5:30 asubuhi . Alisema ,moto huo umeteketeza nyumba hiyo na kwasasa majeruhi hao wanapatiwa matibabu hospitali ya wilaya ya Bagamoyo .

Kamanda Shanna aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni pamoja na Emmanuel Nangu (33) mfanyabiashara ambaye ameungua miguu na mke wake Victoria Mushi (32) aliyejeruhiwa kifuani na mikononi. Mwingine ni msichana wa kazi Jovina Mapinduzi (16) aliyeungua miguuni na mapaja.


Aidha kamanda huyo alisema ,moto huo ulipotokea mitungi miwili ya gesi ilipasuka na kuruka juu na kupasua paa kisha kutoka nje na kuwajeruhi pia wapita njia ambao ni Msafiri Mohammed (36) na Hadija Juma (22) ambaye anuvunjika mguu.

"Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika na kinachunguzwa licha ya kuwa na dhana mbili juu ya moto huo moja ni mitungi ya gesi na tatizo la umeme," alisema Shanna.


Alieleza wananchi wanapaswa kuangalia miundombinu ya umeme kwani baadhi ya nyumba ni michakavu.

"Kikosi cha zimamoto kinapaswa kutoa elimu kwa wananchi ili kutambua mitungi ya gesi ambayo haina matatizo " alifafanua kamanda Shanna.

Kamanda Shanna alisema, shirika la umeme (Tanesco) linapaswa kutoa elimu kwa jamii juu ya kufanya marekebisho ya miundombinu ya umeme kwenye nyumba zao. Aliwaasa wenye nyumba kutoa elimu kwa wadada na wakaka wanaowaweka kufanya kazi kwenye nyumba zao ,ili kujua matumizi ya gesi na vyombo vya umeme.

16 March 2018

March 16, 2018

SHAZILI SAIDI MKUCHI ANATAFUTWA KWA TUHUMA ZA MAUWAJI YA MAMA YAKE MZAZI

Kijana mmoja aitwae Shazili Saidi Mkuchi mkazi wa Mtwara mwenye umri wa miaka 26, anatafutwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mama yake mzazi Bi. Amina Chuwalila kwa kumkata na panga.

Akiongea na mwandishi wa habari kaka wa mtuhumiwa ambaye pia ni mtoto mkubwa wa marehemu anayejulikana kwa jina la Rashidi Saidi Mkuchi, amesema mdogo wake huyo amefanya tukio hilo baada ya kuambiwa na mganga wa kienyeji kuwa mama yake na kaka yake ndiye anayemroga, na kuamua kumfuata shambani alikokuwa na kumfanyia tukio hilo, ambalo limekatisha uhai wake.

“Kama angemkosa mama, basi kifo hiki kingekuwa cha kwangu maana na mimi nimetajwa kuwa nilikuwa nashirikiana na mama yetu kumroga yeye”, amesema kaka wa mtuhumiwa Saidi.

Daktari wa kituo cha afya cha Nanguruwe aliyejulikana kwa jina la Dokta Adam amekiri kumpokea mama huyo akiwa amejeruhiwa vibaya, na kwamba tayari alikuwa ameshafariki.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara Lucas Mkondya amethibitisha kuripotiwa kwa tukio hilo ambalo limetokea Machi 14, na kuwataka wananchi kusaidia kufanikisha kumpata mtuhumiwa huyo ambaye ametokomea kusikojulikana.

Marehem alipokelewa na Dokta Adam wa Kituo cha Afya Nanguruwe na kuthibitisha kuwa alifika Kituoni hapo akiwa tayari Ameshaaga Dunia.
Chanzo :malunde 1 blog
March 16, 2018

Mwandishi aliyekimbilia Finland aijibu Serikali

Mwandishi wa habari Ansbert Ngurumo ameijibu Serikali huku akisisitiza kupata vitisho, ikiwamo kutishiwa maisha kutokana na namna alivyowakosoa viongozi.


Majibu ya Ngurumo yametokana na maelezo ya Serikali kwamba madai ya mwandishi huyo si ya kweli na yamejaa usanii.


Ngurumo ambaye kwa sasa amepewa hifadhi nchini Finland, amedai kwamba Serikali haina rekodi nzuri juu ya watu wanaofuatiliwa na kutekwa ndiyo maana haijui hata Azory Gwanda na Ben Saanane waliko.


Amehoji kama maelezo yake ni usanii wanaotenda maovu ya kuteka na kutesa watu ndani ya nchi, inakuwaje Serikali isijue ni akina nani?


Ngurumo amesema wasamaria ndiyo waliomsaidia kutoroka na kuzijua mbinu za watu waliokuwa wakitaka kumdhulu, hasa katika mikoa ya Mwanza, Kagera na Dar es Salaam ikiwamo kuyatambua magari waliyokuwa wakiyatumia kumfuatilia.


Amesema mbali na kutoa taarifa kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter Oktoba 3, 2017, hakutaka tena kupiga kelele na badala yake aliendelea kupambana kimyakimya, kujilinda na kumulika wabaya wake akiwa mbali.
March 16, 2018

Watanzania watatu wakamatwa Kenya na heroin za Sh1 bilioni


Watanzania watatu wamekamatwa Kenya wakidaiwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin zenye thamani ya Sh1.9 bilioni. Watuhumiwa hao ambao majina yao hayakutajwa walinaswa wakiwa katika hoteli moja mjini Mombasa huku dawa hizo zikiwa zimefichwa katika nguo zilizowekwa kwenye mabegi.

Kwa mujibu wa gazeti dada la Mwananchi, Daily Nation la Kenya, polisi walikuwa wakijiandaa kuwafikisha mahakamani. Waliingia nchini humo kwa usafiri wa basi wakitumia mpaka wa Lunga Lunga. Dawa hizo zinadaiwa kuwa na uzito wa kilogramu 30.

Katika miaka ya hivi karibuni Kenya imekuwa ikichukua mkondo wa mataifa mengine duniani kukabiliana na mitandao inayosafirisha dawa za kulevya. Mapema mwaka uliopita vyombo vya usalama vya Taifa hilo viliwakamata washukiwa 13 wa ulanguzi wa dawa za kulevya mjini Mombasa.

15 March 2018

March 15, 2018

MAMBOSASA: WAKIANDAMANA MITANDAONI HAKUNA TATIZO..BARABARANI WATAJUTA


Kamanda wa jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam Tanzania, Lazaro Mambosasa amefunguka na kusema kuwa kama April 26 mwaka huu watu wataandamana kwa mitandao ya kijamii wao hawana tatizo kwa hilo ila kama wataingia barabarani basi wasijute.


Mambosasa amesema hayo wakati akiongea na kituo cha habari cha kimataifa na kusema kuwa jeshi la polisi limejipanga kuwadhibiti watu ambao watataka kuvunja sheria za nchi kwa kuandamana barabarani. Mambo sasa amesema kuwa jeshi hilo limejipanga vizuri hivyo wanawakaribisha wale ambao watahamisika kuandamana barabarani.


"Ndani ya kanda mimi nasema hakuna maandamano wanahamasishana wanapotezeana muda na wamezoea kufanya hivyo na walitishia kufanya hivyo wakati uliopita lakini tunachosema tumejipanga vizuri sisi ni wasimamizi wa sheria atakayetaka kuvunja sheria atapambana na sisi lakini asijutie matokeo ya kile atakachokutananacho, wakiandamana kupitia mitandao ya kijamii manake hakuna tutakaokutana nao barabarani hivyo wataandamana kwa kuendelea kupeana habari kwenye mitandao na hilo sisi hatuna shida ndio maana tunaendelea kupuuza yanayopangwa lakini yoyote atakayehamasika kupitia mtandao akaja barabarani kwa maana ya kuleta vurugu kuvunja sheria za nchi tutakutana naye tumejipanga"


Mambosasa aliendelea kusema kuwa


"Ulinzi upo tu unataka kujua kiasi gani tumejipanga kwa namna gani? Sisi tupo vizuri katika hilo na tunakukaribisha barabarani kama unataka kuandamana na wewe" alisisitiza Mambosasa


Mange Kimambi amekuwa akihamasisha sana watu kupitia mitandao ya kijamii kuandamana katika siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo kila mwaka sherehe hizo huwa zinafanyika tarehe 26 mwezi wa nne.
March 15, 2018

MMILIKI WA MABASI YA SUPER SAMI AKUTWA AMEKUFA MTONI


Mwili wa Mmiliki wa mabasi ya Super Sami Samson Josiah umekutwa katika mto Ndabaka eneo la Bunda /Lamadi.


Taarifa kutoka vyanzo vya habari vya Malunde1 blog ni kwamba mwili wa Samson Josiah umeokotwa na wavuvi wa samaki leo jioni Jumatano Machi 14,2018.


Watu wa karibu na marehemu wanasema mwili uliookotwa ni wa Samson Josiah.

14 March 2018

March 14, 2018

Droo kwa ajili ya mechi za robo fainali Klabu Bingwa Ulaya kufanyika kesho ijumaa mjini Nyon nchini Uswisi.Droo kwa ajili ya kupanga mechi za robo fainali za klabu bingwa Ulaya inatarajiwa kufanyika kesho ijumaa katika makao makuu ya UEFA mjini Nyon nchini Uswisi majira ya saa nane mchana kwa saa za Afrika Mashariki.

Timu nane zitakazopambanishwa katika droo hiyo ni Barcelona (Hispania), Bayern M√ľnchen (Ujerumani), Juventus (Italia), Liverpool (Uingereza), Manchester City (Uingereza)

Real Madrid (Hispania), Roma (Italia) na Sevilla (Hispania).

Mechi za robo fainali zinatarajiwa kupigwa tarehe 3 na 4 mwezi Aprili, ikiwa ni mechi za awali, na marudiano tarehe 10 na 11 mwezi Aprili.
March 14, 2018

Carrick atangaza kustaafu sokaKiungo wa Manchester United, Michael Carrick ametangaza kustaafu soka baada ya msimu huu kumalizika.

Carrick alijiunga na Manchester United mwaka 2006 akitokea Tottenham Hotspurs kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 18 huku akicheza michezo 468.

Kufuatia kauli hiyo, kocha wa Man U, Jose Mourinho amesema atafurahi kuona Carrick akistaafu soka kisha aendelee kusalia ndani ya timu hiyo kwa majukumu mengine ya kazi.
March 14, 2018

Sheria hairuhusu wimbo uliofungiwa kuufanyia show nje ya nchi – Naibu WaziriNaibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Juliana Shonza amesema sheria hairuhusu wimbo uliofungiwa nchini kutumika katika show nje ya nchi.

Naibu Waziri amesema hayo leo kupitia kipindi cha XXL cha Clouds ambacho kuliwakutanisha wasanii, wizara na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA).

“Sheria hairuhusu wimbo wa msanii husika uliofungiwa hapa Tanzania kwenda kuufanyia show nje ya nchi. Endapo atafanya hivyo atakuwa anakiuka kanuni na sheria za nchi.” amesema Juliana Shonza.

February 28 mwaka huu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilipokea list ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka kwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) na kuamuru kutopigwa katika vyombo vya habari.